Habari za michezo

CHAMA AZUA GUMZO CCM KIRUMBA …..AFUNGA MJADALA KUHUSU MGOGORO KATI YAKE NA PABLO…

admin May 22, 2022 2:37 pm


Presha imetulia, ndivyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki wa Simba kuibua shangwe na kuondoa wasiwasi baada ya kumshuhudia nyota kipenzi wa timu hiyo, Clatous Chama katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Chama hajaonekana kikosini hapo kwa muda mrefu hivyo kuibua wasiwasi kwa mashabiki kutokana na minong’ono kuwa hana maelewano na benchi la ufundi.

Baada ya kutoonekana jana na kikosi hicho katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika uwanja wa CCM Kirumba hatimaye leo Chama ameonekana na kushangiliwa kwa nguvu.

Mzambia huyo aliongozana na wenzake kwa kutumia basi la timu hiyo lililowasili uwanjani hapo saa 8:28 mchana.

Baada ya mastaa wote kushuka kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo huku mashabiki wakijua hayupo hatimaye alishuka na kuwapungia mikono jambo ambalo limeibua shangwe kubwa.

Baada ya kuwasalimia mashabiki Chama alirudi kwenye gari pamoja na Meneja habari wa timu hiyo, Ahmed Ally ambapo  aliendelea kukaa kwenye gari hilo lililopaki uwanjani hapo.

KUELEKEA MECHI YA KESHO NA BIASHARA UNITED…NABI ASHTUKA…AUKWEPA MTEGO WA SIMBA UWANJA WA CCM KIRUMBA…. FT: GEITA 1-1 SIMBA SC ….MPOLE AZIDI KUTAKATA…KIBU AWAOKOA NA AIBU YA KIPIGO…YANGA SASA BADO NNE TU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply