Habari za michezo

ZA NDANIII KABISA….BAADA YA MORRISON KUPIGWA CHINI….MOSES PHIRI IMEBAKI TIKETI YA NDEGE TU ATUA ZAKE BONGO…

admin May 22, 2022 11:32 pm


HABARI njema kwa mashabiki wa Simba ni usajili mpya ndani ya timu hiyo ambao kwa kiasi kikubwa dili limekamilika, huku akitajwa kuwa ndiye atachukua nafasi ya Bernard Morrison kwa wachezaji wa kimataifa.

Usajili huo ni mshambuliaji Moses Phiri raia wa Zambia ambaye anajiunga na Simba msimu ujao akitokea Zanaco ya nchini kwao.

Inaelezwa kwamba, Phiri atakuwa mchezaji wa kwanza kutua Simba kwa wale wapya ambao watajiunga na timu hiyo msimu ujao kutokana na kila kitu kikamilika, anasubiri tiketi tu ya ndege atumiwe ili atue Dar.

Chanzo chetu kutoka Zambia, kimethibitishia  juu ya Simba kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Yanga.

“Moses Phiri kwa sasa ni mali ya Simba, kulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu baina ya uongozi wa Moses Phiri na Simba jambo ambalo makubaliano yalishafikiwa na sasa rasmi mchezaji huyo ni mali ya Simba.

“Mchezaji mwenyewe tayari alishakubali kutua Simba ambapo kigezo kikubwa cha kukamilisha dili la kujiunga na Simba ni kutokana na uwepo wa Wazambia wenzake kama Chama (Clatous) na Bwalya (Rally),” kilisema chanzo hicho.

Tulipomtafuta wakala wa mchezaji huyo, Nyambe Nawa kuhusu dili hilo, alisema: “Kuna asilimia kubwa ya Phiri kucheza Tanzania msimu ujao, hivyo ni suala la muda kwa sasa na kila kitu kitakuwa wazi.”

KUELEKEA MECHI YA NUSU FAINALI SHIRIKISHO…MAYELE AIBUKA NA HILI KWA SIMBA…ATOA AHADI YA AJABU… TUKIO LA MANULA KUTOKWA DAMU MKONONI GHAFLA KABLA YA MECHI YA JANA…ISHU NZIMA KUMBE IKO HIVI…SHABIKI ATAJAWA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply