Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA YANGA vs SIMBA JUMAMOSI HII…TFF ‘YAWACHINJILIA MBALI’ MABASHABIKI WA BUKU 5…

admin May 24, 2022 5:15 pm


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga na Simba Jumamosi Mei 28, 2022 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo, kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 10,000 kwa eneo la mzunguko, wakati VIP B ni Sh. 20,000 na VIP A Sh.30,000.

Hii ni sawa na kusema kuwa mashabiki waliozoea kwenda uwanjani na kununua tiketi za tsh elfu 5 safari hii wamechinjiwa baharini.

Mchezo huu utakuwa ni wa tatu kwa msimu huu na wapili kwa mwaka huu, ambapo katika mechi ya kwanza ambayo ilikuwa ya Ligi iliyocheza mwezi uliopita timu hizi zilitoka suluhu.

Simba wataingia katika mchezo ujao wakiwa na historia ya kutokupata ushindi kwenye mechi mbili zilizopita walizocheza na watani zao Yanga.

Huku Yanga wao wataingia uwanjani wakiwa na morali ya matokeo ya kwenye ligi kuu, pamoja na ushindi wa mechi ya kwanza timu hizi zilipokutana kwenye mchezo wangao ya jamii.

Timu yeyote itakayoshinda mechi hio, inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho msimu huu, ambapo Simba itakuwa ni mara yake ya nne, wakati Yanga wao hawajawahi kushinda taji hili.

KISA WACHEZAJI WA TANZANIA KUKAGULIWA SEHEMU ZA SIRI….TFF WASHINDWA KUJIZUIA…WAKIMBILIA CAF HARAKA… COASTA UNION WAZILIPIZIA KISASI SIMBA NA YANGA KWA MBEYA CITY…’WAIKAANGA CHA UCHUNGU’ …POLISI WAINGILIA KATI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply