Habari za michezo

MBAPPE AFICHUA ALIVYOITOSA LIVERPOOL….PAMOJA NA MAMA YAKE KUINGILIA KATI LAKINI WALITOKA ‘KAPA’….

admin May 24, 2022 1:38 pm


Nyota Kylian Mbappe amekiri kufanya mazungumzo na klabu ya Liverpool kabla hajasaini mkataba wa kujiunga na wababe wa Paris klabu ya PSG mnamo msimu wa 2017/18 akitokea kwa klabu ya As Monaco kwa mkopo .

Mbappe mwenye umri wa miaka 23 aliyeongeza kandarasi mpya ndani ya klabu ya PSG mpaka 2025 amesema alikutana na maofisa wa klabu ya Liverpool miaka 5 iliyopita akiwa bado anacheza katika klabu ya Monaco mnamo mwaka 2017.

“tulifanya mazungumzo japo hayakuwa marefu, Liverpool ni klabu kubwa na yenye historia ndani yake lakini pia  mama yangu anaipenda klabu hiyo na sijui kwanini anaipenda klabu hiyo kwa maana mnapaswa kumuuliza yeye mwenyewe lakini mwishoni ilikuwa nichague kucheza kati ya Real Madrid au Paris Saint Germain ”amesema Mbappe

Vilabu vya Real Madrid na Liverpool watacheza mchezo wa fainali wa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya(Uefa Champions League) kwa msimu wa 2021/22 mnamo Mei 28,2022 kwenye jiji la Paris,Ufaransa

BAADA YA SIMBA ‘KUMTEMA KISAILENSA’….MORRISON KAONA ISIWE TABU…KAAMUA KUJA NA HILI JIPYA MJINI… UKWELI MCHUNGU….UBINAFSI WA SAKHO NA ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU…HUWA ANAJIANGALIA YEYE ZAIDI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply