Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, amesema ana nia ya kuichezea klabu hiyo msimu ujao licha ya kuwa amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake.
Mkataba wa sasa wa Mohamed Salah ndani ya Liverpool unamalizika 2023, na amesema atakuwa Anfield msimu ujao lakini atavutiwa zaidi iwapo atasaini mkataba mpya.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri bado yuko kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu mkataba mpya, ingawa ripoti zinaonyesha kuwa makubaliano bado hajafikiwa.
Salah amefunga mabao 31 na kutoa asisti 15 katika mechi 50 katika michuano yote msimu huu, kulikua na baadhi ya ripoti zikimhusisha na kuhama mwishoni mwa msimu huu.
Lakini amezungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid Jumamosi, Salah aliweka wazi kuwa ana nia ya kusalia Anfield kwa angalau mwaka mmoja zaidi,:
“Ninasalia msimu ujao kwa hakika.”
Salah hapo awali alisema hataki kuzungumzia hali ya mkataba wake hadi mwisho wa msimu, na alisisitiza msimamo huo na kuongeza: “Katika mawazo yangu, siangazii mkataba, sitaki kuwa na ubinafsi, hii ni wiki muhimu kwetu. Sitaki kuzungumzia mkataba.”