Habari za michezo

ILE ISHU YA CHAMA KURUDISHWA DAR WAKATI WENZAKE WAKIJIANDAA NA YANGA MWANZA KUMBE CHANZO NI HIKI…

admin May 26, 2022 4:55 pm


Kiungo mshambuliaji wa kikosi cha Simba Clatous Chama hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachowakabili Yanga Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza baada ya jana kuondoka kambini.

Inaelezwa Chama alienda Mwanza lakini hakuwa fiti baada ya kupata majeraha siku kadhaa zilizopita huku akiruhusiwa kurejea Dar es Salaam jana.

Baada ya Simba kutua Mwanza Chama alianza mazoezi na wenzake lakini juzi alipelekwa hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi na kubaini anahitajika matibabu zaidi.

Mbali na kurejea Dar es Salaam nyota huyo amepewa ruhusa ya kwenda nchini kwao Zambia kushiriki mwaka mmoja wa kifo cha marehemu mke wake aliyefariki dunia Mei 28 mwaka jana.

KUHUSU ISHU YA KUTEMANA NA YANGA…NTIBAZONKIZA APANGA KUTAPIKA NYONGO…”SITARUHUSU MTU ANICHAFUE”… KUHUSU KUBAKI AU KUSEPA LIVEPOOL MSIMU UJAO …SALAH KAVUNJA UKIMYA…KAFUNGUKA ANACHOHITAJI KWA SASA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply