Home Habari za michezo NDOTO ZA MORRISON KWA GHANA ZAZIDI KUPOTEA…AWEKWA KANDO MAZIMA…HAWANA HABARI NAYE KABISA...

NDOTO ZA MORRISON KWA GHANA ZAZIDI KUPOTEA…AWEKWA KANDO MAZIMA…HAWANA HABARI NAYE KABISA YANI…


Licha ya mara kadhaa kulalamikia kutoteuliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana ‘Black Star’, mshambuliaji Bernard Morrison ameendelea kufungiwa vioo na benchi la ufundi la timu hiyo.

Kocha wa Black Star, Otto Addo hajamjumuisha Morrison katika kikosi chake alichokitangaza leo kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (Afcon) 2023 mapema mwezi ujao dhidi ya Madagascar na Afrika ya Kati.

Juni Mosi, Ghana itaikaribisha Madagascar na baada ya hapo itakuwa ugenini kukabiliana na Afrika ya Kati, Juni 5.

Morrison ni miongoni mwa wachezaji wa Ghana ambao hawajaitwa na kocha Addo kwenye kikosi hicho chenye kundi kubwa la nyota wanaocheza soka la kulipwa nje ya Bara la Afrika.

Kiwango bora alichoonyesha kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ambalo timu yake Orlando Pirates ilifika fainali, kimemfanya Kipa Richard Ofori kuendelea kujumuishwa kundini.

Nyota wa Al Sadd, Andre Ayew ataendelea kuongoza timu hiyo kama nahodha lakini msaidizi wake Thomas Partey wa Arsenal ambaye ni majeruhi hajajumuishwa.

Kikosi hicho kinaundwa na makipa, Jojo Wollacott- (Swindon Town), Abdul Manaf Nurudeen (Eupen), Lawrence Ati-Zigi (St. Gallen) na Richard Ofori (Orlando Pirates)

Mabeki ni Denis Odoi (Club Brugge), Alidu Seidu (Clermont Foot), Gideon Mensah (Bordeaux), Abdul Baba Rahman (Reading), Abdul Mumin (Vitoria Guimaraes), Daniel Amartey (Leicester City),  Joseph Aidoo (Celta Vigo) na  Jonathan Mensah (Columbus Crew).

Kwa upande wa viungo, walioitwa ni Iddrisu Baba(Mallorca), Edmund Addo (Sheriff Tiraspol), Elisha Owusu (KAA Gent), Mohammed Kudus (Ajax), Daniel Kofi Kyereh (St. Pauli) na  Mubarak Wakaso (Shenzhen).

Wengine ni Joseph Paintsil (Genk), Andre Ayew (Al Sadd),  Augustine Okrah (Bechem United), Osman Bukari (Nantes), Abdul Fatawu Issahaku (Sporting CP), Kamaldeen Sulemana (Stade Rennes), Yaw Yeboah (Columbus Crew) na  Christopher Antwi-Adjei (Bochum).

Washambuliaji ni Jordan Ayew(Crystal Palace), Daniel Afriyie (Hearts of Oak), Felix Afena Gyan (AS Roma), Kwesi Okyere Wriedt (Holstien Kiel),  Antoine Semenyo (Bristol City),  Benjamin Tetteh (Yeni Malatyaspor) na  Braydon Manu (SV Darmstadt).

SOMA NA HII  KISA KUSHINDWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA...KOCHA TAIFA STARS AELEKEZA LAWAMA ZOTE HUKU..