Habari za michezo

PAMOJA NA KUWA NA MSIMU M’BOVU….MASHABIKI MAN UTD WAONYESHA UBABE…WANUNUA TIKETI ZOTE …..

admin May 28, 2022 7:09 am


Ama kweli, mkubwa ni mkubwa. Licha ya kuwa na msimu mbovu 2021/22, Manchester United imeshauza tiketi zote za msimu ujao, 2022/23.

Old Trafford ni uwanja mkubwa zaidi Uingereza unaomilikiwa na klabu. Ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 74,000, Man United mara zote inawekaga tiketi zaidi ya 50,000 kwa ajili ya mashabiki wanaonunua tiketi za msimu mzima.

Ikiwa ni juzi tu msimu umeisha na Jana Erik Ten Hag kuanza majukumu yake rasmi kama kocha mkuu wa United, klabu hiyo imetangaza kumaliza mauzo ya tiketi kwa mashabiki wanaonunua tiketi za msimu mzima.

Hii ni nguvu ya ajabu ambayo, mashabiki wa klabu hiyo wamekua nayo wakionesha mapenzi makubwa kwa timu yao licha ya kuwa katika nyakati ngumu kwenye kupata matokeo.

2022 ni mwaka wa 9 toka The Red Devils walipotwaa taji la EPL na, hata hivyo ukame wa makombe umeendelea toka Sir Alex Ferguson alipostaafu kuiongoza klabu hiyo. 2022/23 utakua msimu wa aina gani chini ya Ten Hag?

YANGA MAFIA SANA AISEE…NTIBAZONKIZA NDIO BASI TENA JAGWANI…ASEPA JUMLA JUMLA NA KILA KITU CHAKE… PAMOJA NA KUSAJILIWA KWA MATARAJIO MAKUBWA…AJIBU MAJI YA SHINGO AZAM FC….APIGWA CHINI MAZIMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply