Habari za michezo

BAADA YA KUIFANYIZIA SIMBA JANA….YANGA WATUA DAR KAMA WOTEE….MSTAA NANE WATIMKA CHAPCHAP…

admin May 29, 2022 11:52 am


BAADA ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kikosi cha Yanga kimetua jijini Dar es Salaam na kupewa ruhusa ya mapumziko ya siku nne huku wachezaji nane wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ wakitinga moja kwa moja kambini.

Yanga walitinga hatua ya fainali kombe la Azam Shirikisho  kwa kuwafunga watani zao Simba bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza likifungwa na Feisal Salum.

Timu ikiambatana na benchi la ufundi na viongozi waliwasiri uwanja wa ndege saa 3:30 asubuhi na kupokelewa na mashabiki wachache waliojitokeza huku wakitaja jina la Feisal Salim ‘Fei Toto’.

Baada ya kutua basi dogo la kijivu ikiwa na viongozi wa TFF waliwataka mastaa wote walioitwa timu ya Taifa kupanda ndani ya gari hiyo tayari kwa ajili ya kambi kujiandaa na mechi mbili za kufuzu AFCON 2023.

Wachezaji wakiongozwa na nahodha wao Bakari Mwamnyeto walijaribu kuomba ruhusa ili kuziona familia zao waligomewa na kuamuliwa wapande ndani ya gari hiyo.

Wachezaji walioitwa na kwenda kambini ni Mwamnyeto, Fei Toto, Abubakar Salum ‘Sure Boy’, Aboutwalib Mshery, Dickson Job, Kibwana Shomari, Farid Mussa na Zawadi Mauya.

BAADA YA GOLI LAKE LA TIKITAKA KUCHAGULIWA KUWA BORA CAF MSIMU HUU…PAPE SAKHO APEWA UBALOZI SENEGAL…. HIVI NDIVYO JINSI FAINALI YA JANA YA LIGI YA MABINGWA ULAYA ILIVYOWACHA LIVERPOOL NA MACHOZI YA DAMU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply