Habari za michezo

BAADA YA SIMBA KUPUKUTISHWA NA YANGA MSIMU HUU…AHMED ALLY AVUNJA UKIMYA…AMWAGA UKWELI WOTE HADHARANI…

admin May 30, 2022 3:04 am


Meneja wa mawasiliano Simb SC, Ahmed Ally amesema kuwa watayafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza msimu huu ikiwemo kukiboresha kikosi chao.

”Hatuna namna tujipange kwaajili ya msimu ujao, kitu ninachoweza kuwaahidi wanasimba ni kwamba tumeshaona ni wapi kwenye mapungufu, wapi panamatatizo tuna waahidi kwamba tunakwenda kufnya maboresho makubwa ndani ya timu yetu, tunakwenda kufanya usajili mkubwa wa timu yetu ili kuhakikisha kwamba msimu ujao hatupitii mateso tunayopitia msimu huu.”

Simba SC msimu huu imeshindwa kutimiza hata lengo moja kati ya yale matatu waliyojiwekea mbele ya Kocha Pablo, ikiwemo kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho, kuchukua kombe la Azam Sports Federation Cup pamoja na Ligi Kuu.

Hata hivyo Simba imeonekana kutofurukuta anapokutana na mtani wake Yanga SC msimu huu ikiwemo kupoteza Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup na Ngao ya Jamii.

WAZAZI WALIOMPA MTOTO WAO MCHANGA JINA LA MAYELE WAFUNGUKA…”SIWEZI KUMBADILISHA JINA HATA IWEJE”… PABLO AKALIA KUTI KAVU…SIMBA WAANZA MAZUNGUNZO NA KOCHA WA RAJA CASABLANCA…MORRISON AAGA RASMI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply