Habari za michezo

KIMEUMANA SIMBA….RAGE AMSHUKIA MO DEWJI JUMLA JUMLA…ATAKA BARBRA NA WENZAKE WATIMULIWE…

admin May 30, 2022 2:52 pm


Mwenyekiti wa zamani Simba, Ismail Aden Rage amemtaka Mwekezaji wa Klabu hiyo Mohamed Dewji (Mo) kuivunjilia mbali Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kwani imejaa wababaishaji.

Rage akizungumza leo siku moja baada ya kauli ya Mwekezaji huyo kusema kuwa kuna haja ya kuifumua timu yao nzima na kuisuka upya, ametaka hilo lifanyike kwanza kwa kuivunja Bodi hiyo ya Wakurugenzi kwani haina watu wa kweli wa mpira bali wanamdanganya tu.

Kwa kuweka taarifa sawa, Bodi hiyo ya Wakurugenzi, pamoja na kuwa na wajumbe wengine pia Mtendaji Mkuu wa Klabu Bi Barbara Gonzalez ni sehemu ya wanaounda bodi hiyo.

Kwa Mantiki hiyo, Rage amemaanisha wanaopaswa kufukuzwa Simba ni pamoja na Barbara.

Rage amesema haoni pia sababu ya kocha wa Pablo Franco kutimuliwa bali kwanza waanzie kwenye bodi ya Klabu hiyo.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Yanga jana katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Azam huko Mwanza na kuvuliwa ubingwa wa Kombe hilo.

NI MO DEWJI TENA….ATUMIA ‘TWEETER’ YAKE KUJIBU MAPIGO …ASHUSHA ‘NONDO ZA MAANA’ KUHUSU SIMBA… BAADA YA KUPANDA LIGI KUU KWA MSIMU UJAO…DTB FC WABADILI JINA ….MCHAKATO MZIMA UKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply