Habari za michezo

BAADA YA KUTINGA FAINALI….BILIONEA WA COASTAL UNION YA TANGA AIPIGA MKWARA YANGA SC..

admin May 31, 2022 1:50 am

 


Mdau wa Soka mkoani Tanga Nassor Bin Slum ameitahadharusha Young Afrivans kwa kuitaka ijipange kuelekea mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Coastal Union imejihakikishia kucheza Fainali ya michuano hiyo leo Jumapili (Mei 29), baada ya kuichapa Azam FC kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 6 kwa 5, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Bin Slum ambaye aliwahi kuidhamini Coastal Union ametoa tahadhari kwa Young Africans, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, dakika chache baada ya mpira kumalizika jijini Arusha.

Bin Slum ameandika: “Yanga mjipange tunakuja, This is New Coastal Union under Guardiola Mnene…..Kama wewe ni shabiki wa Mangush piga keleleee”

Young Africans ilitangulia Fainali jana Jumamosi (Mei 28), kwa kuifunga Simba SC 1-0 jijini Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo wa Fainali utapigwa Julai 02 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao juzi Jumapili (Mei 29) umetumika kwa mchezo wa Nusu Fainali.

MORRISON AVUNJA UKIMYA SAKATA LA KUFUKUZWA SIMBA…ADAI BARBARA NDIO HAMTAKI…SIMU ZAKE HAZIPOKELEWE… ISHU YA BWALYA NA MZAMIRU….HATIMA YAO KUAMULIWA NA MASHABIKI WA SIMBA…KIBU DENISI NAYE NDANI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply