Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUFANIKIWA KUMZUIA MAYELE JUZI’…. SIMBA KUKUTANA NA ‘CHUMA CHA PUA’...

BAADA YA ‘KUFANIKIWA KUMZUIA MAYELE JUZI’…. SIMBA KUKUTANA NA ‘CHUMA CHA PUA’ LUSAJO….


Klabu ya soka ya Simba imetua rasmi mkoani Mtwara tayari kuwakabili Namungo FC katika pambano la Ligi Kuu ya NBC kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 3 2022 katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja bila kwenye mchezo wa awali ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam bao lililofungwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika za majeruhi.

Kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Simba ipo katika nafasi ya pili ikiwa na jumla ya alama 42 alama 13 nyuma ya vinara Yanga ambao wana jumla ya alama 55 lakini Simba ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mchezo wa kesho ni muhimu kwa timu zote mbili kwani Namungo FC ikipoteza mchezo huo kimahesabu itakuwa tayari imejitoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu huku Simba nayo inalazimika kushinda ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wake.

SOMA NA HII  MO DEWJI ATIBUA DILI LA GOMES KWENDA RAJA CASABLANCA YA MOROCCO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here