Home Habari za michezo BAADA YA KUMCHUKUA MIQUISSONE….AL ALHY WARUDI TENA SIMBA…WAMTAKA SAKHO…ISHU NZIMA IKO HIVI…

BAADA YA KUMCHUKUA MIQUISSONE….AL ALHY WARUDI TENA SIMBA…WAMTAKA SAKHO…ISHU NZIMA IKO HIVI…


MABINGWA watetezi wa soka Afrika, Al Ahly na Orlando Pirates ni kati ya timu zinazotajwa kumuwinda kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Senegal, Pape Sakho.

Klabu ya Simba imethibitisha kuwindwa kwa mchezaji huyo, ingawa imesema bado ana mkataba mrefu na klabu hiyo, lakini ikaongeza kuwa hakuna mchezaji asiyeuzwa duniani.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema siyo timu hizo tu, bali mchezaji huyo amekuwa akiuliziwa na klabu mbalimbali Afrika na nje ya bara hili kwa ajili ya kupata huduma yake.

“Ingekuwa ni ajabu sana kama Sakho mkapa sasa asihusishwe na klabu yoyote ile, na sisi kama Simba tungekuwa tumefeli. Siyo Al Ahly tu, hata Orlando nayo inemuulizia, kwa sababu kiwango alichonacho hakuna klabu yoyote yenye kutaka mafanikio isitamani kuwa naye, kwa hiyo watu wasishangae kusikia anauziliwa, ni kwa sababu ana ubora,” alisema Ahmed.

Alisema kuwa msimamo wa Simba ni kwamba wasingependa kuwa wanauza wachezaji wao, ila wakati mwingine huwa zinakuja ofa nono ambazo huwa zinaitingisha klabu na mchezaji mwenyewe.

“Kama itakuja ofa nzuri vya kutosha, tukaona tukimwachia tunaweza kupata Sakho mwingine kwa bei zuri, tutafanya hivyo, wakati tunamuuza Miquissone (Luis) watu hawakujua kama atapatikana mbadala mwingine wa kufanya vizuri, akaja Sakho. Mpira ni biashara, unauza na kununua, na hakuna mchezaji duniani asiyeuzwa, maulizo ya mchezaji huyu yako mengi, lakini ikumbukwe kuwa bado ana mkataba na Simba,” alisema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWATAZAMA YANGA...KOCHA WA USM ALGER KANUGA WEE..KISHA AKASEMA HAYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here