Home Habari za michezo BAADA YA KUONA UKAME WA MAGOLI UNAMZIDI…MAYELE AIBUKA NA HILI YANGA…AAMUA KUJIWEKA...

BAADA YA KUONA UKAME WA MAGOLI UNAMZIDI…MAYELE AIBUKA NA HILI YANGA…AAMUA KUJIWEKA KANDO….


Baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Dodoma Jiji ambao Yanga ilishinda mabao 2-0 huku Fiston Mayele akiwa hajaingia wavuni, mwenyewe amewatuliza mashabiki.

Mayele aliwaambia mashabiki wa Yanga kwamba; β€œBado tuna mechi, zinanitosha kutetema. Sasa hivi tunachoangalia ni mafanikio ya timu kwanza, hayo mengine yatakuja baadaye.”

β€œKuna malengo ya timu na mtu binafsi ambaye ni mchezaji, timu kwanza mambo mengine baadaye. Bado malengo yangu ya kuwa mfungaji bora yako palepale na muda ninao. Mechi bado zipo mashabiki wasiwe na wasiwasi.”

Toka mechi dhidi ya Simba, Mayele ambaye amekuwa mkombozi wa Yanga msimu huu, hajafanikiwa kufunga goli la aina yeyote ile katika mechi za Ligi Kuu.

SOMA NA HII  YANGA:- MMILIKI WA IHEFU KAUZIWA MZIGO WA BANGI.....