Home Habari za michezo BODI YA LIGI YAMSHUKIA JUMLA JUMLA MASOUD DJUMA KWA KUPIGANA MATEKE NA...

BODI YA LIGI YAMSHUKIA JUMLA JUMLA MASOUD DJUMA KWA KUPIGANA MATEKE NA MCHEZAJI WAKE…


Kocha wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma na mchezaji wa timu hiyo Jamali Mtegeta wamefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh 500,000 kila mmoja kwa kosa la kushambuliana kwa mateke wakati mchezo dhidi ya Biashara United ukiendelea kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Kocha Masoud Djuma alimpiga teke mchezaji Jamali Mtegeta aliyekuwa kwenye benchi kabla mchezaji huyo hajarejesha pigo la aina hiyo kwa kocha wake.

Masoud Djuma ambaye amerudi Tanzania kw amara ya pili na kufanikiwa kupata ajira kwenye timu hiyo, bado hajaweza kuwa na matokeo ya muendelezo wa ushindi tangia alipopata kibarua cha kuifundisha timu hiyo.

SOMA NA HII  TECNO YAZINDUA SIMU MPYA KALII YA CAMON 19... YENYE KUPIGA PICHA KALI HASA USIKU....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here