Home Habari za michezo FT YANGA 0-0 TZ PRISONS….MAYELE ANAZIDI KUPOTEANA ‘JAMENI’….GUNDU LA SIMBA LAIGANDA YANGA…

FT YANGA 0-0 TZ PRISONS….MAYELE ANAZIDI KUPOTEANA ‘JAMENI’….GUNDU LA SIMBA LAIGANDA YANGA…


Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ukishuhudiwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Tanzania Prisons ukimalizika kwa sare tasa.

Mchezo huo ambao Yanga waliutawala tangu dakika ya kwanza, umemalizika kwa sare kutokana na Yanga kushindwa kutumia vyema nafasi ambazo wamezitengeneza.

Fiston Mayele aliikosesha Yanga ushindi mara baada ya kushindwa kupachika nyavuni mkwaju wa penati iliyopatikana baada ya kufanyiwa madhambi kwa kiungo Feisal Salum.

Yanga wanakamilisha mechi ya tatu mfululizo hii leo ambapo wanacheza pasipo kuibuka na ushindi, gundu la kupata matokeo haya lilianza kwenye mechi dhidi ya Simba, likaamia kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting na sasa mechi ya leo dhidi ya Tanzania Prisons

Kwa sare hiyo Yanga wanafikisha alama 57 na kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi huku Prisons wao wakifikisha alama 23.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA WENZAKE WAKIZIDI 'KUSHINE' ...PHIRI 'AFOSI' JAMBO SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here