Home Habari za michezo FT: YANGA SC 4-0 MBEYA KWANZA…HATIMAYE MAYELE KAONA MWEZI…BADO POINTI SITA TU...

FT: YANGA SC 4-0 MBEYA KWANZA…HATIMAYE MAYELE KAONA MWEZI…BADO POINTI SITA TU KISHINDO KILIE JANGWANI…


Dakika 90 zinakamilika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam huku Yanga wakiondoka na alama tatu muhimu.

Yanga wameitandika timu inayoburuza mkia katika msimamo wa Ligi, Mbeya Kwanza magoli 4-0.

Magoli ya Yanga Matatu yamefungwa Kipindi cha Kwanza na Fiston Mayele, Ntibazonkiza na Dickson Ambundo.

Kipindi cha Pili Mshambuliaji Heritier Makambo aliwafungia Yanga goli la nne na kuwahakikishia alama tatu.

Ushindi huo unawafanya Yanga kufikisha alama 63, huku wakihitaji alama 6 tu kujitangazia ubingwa katika michezo mitano waliyobakisha.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI YA KARIAKOO...LWANGA NA MUGALU 'OUT' SIMBA...PABLO AKATAA VISINGIZIO...ADAI HAIWEZEKANI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here