Home Habari za michezo HIZI HAPA REKODI KIBAO AMBAZO LIVERPOOL WALIWEKA JANA BAADA YA KUFUZU FAINAL...

HIZI HAPA REKODI KIBAO AMBAZO LIVERPOOL WALIWEKA JANA BAADA YA KUFUZU FAINAL UEFA…


Klabu ya Liverpool ya England imefuzu fainali ya Ligi ya mabingwa barani ulaya kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2 dhidi ya Villarreal ya Hispania kwenye michezo miwili ya hatua ya nusu fainali. Hii ni mara baada ya kushinda mchezo wa mkondo wa pili jana usiku kwa mabao 3-2.

Katika mchezo wa usiku wa jana timu hizi ziligawana vipindi ambapo Villarreal walitawala kipindi cha kwanza na walitangulia kufunga mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza kupitia kwa Boulaye Dia na Francis Coquelin na Liverpool wakauchukua mchezo kipindi cha pili wakafanikiwa kufunga mabao 3 kupitia kwa Fabinho, Luiz Diaz na Sadio Mane ambaye kafikisha mabao 21 msimu huu.

Hii ni fainali ya tatu ya Ligi ya mabingwa kwa kocha Jurgen Klopp anafuzu akiwa na kikosi cha Liverpool, na katika fainali mbili zilizopita ametwaa ubingwa mara moja lakini pia hii itakuwa ni fainali yake ya 4 kama kocha fainali moja alicheza akiwa kocha wa Borussia Dortmund ya Ujerumani. Na anaungana na Makocha wengine walicheza fainali 4  za michuano hii ambao ni Marcelo Lippi, Carlo Ancelotti na Sir Alex Ferguson.

Hii pia ni mara ya 10 Liverpool wanafuzu fainali ya Ligi mabingwa, ikiwa ni timu ya 4 kucheza fainali kuanzia 10, wanaungana na Real Madrid waliocheza fainali 16, AC Milan fainali 11 na Bayern Munich fainali 11. Majogoo hao pia ni timu ya kwanza England kucheza fainali ya Kombe la Ligi (Carabao Cup), FA CUP na UEFAChampions League ndani ya msimu mmoja.

Na katika hatua ya fainali watacheza na mshindi wa mchezo wa nusu fainali inayowakutanisha Manchester City na Real Madrid. Na mchezo huu unachezwa leo Usiku uwanja wa Santiago Bernabeu ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili. Manchester City wataingia kwenye mchezo huu wakiwa wanaongoza kwa mabao 4-3 ushindi waliopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

SOMA NA HII  ILI KUEPUKANA NA 'FIGISU FIGISU' ZA YANGA....WASAUZI WAAMUA 'KUUCHUNA'...'WASUSA' KILA KITU BONGO...