Home Habari za michezo KISA ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU…AHMED ALLY AENDELEA KUTOA ‘MAHUBIRI YA FARAJA’...

KISA ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU…AHMED ALLY AENDELEA KUTOA ‘MAHUBIRI YA FARAJA’ INSTAGRAM…AWASHUKIA WENYE CHUKI…


Meneja wa Habari na Mwasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amewashukia baadhi ya wadau wa Soka wanaotumia kipindi hiki kutaka kuvuruga utulivu na amani ndani ya klabu hiyo, kwa kigezo cha kupoteza mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Simba SC ilipoteza muelekeo wa kutetea taji la ‘ASFC’ Jumamosi (Mei 28) kwa kukubali kufungwa 1-0 na Young Africans, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ahmed Ally amewataka Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuhakikisha wanaendelea kuwa kitu kimoja kama ilivyokua kabla hawajapoteza Ubingwa.

Amesema wanaotumia kipindi hiki kupenyeza Chuki zao kwa kutoa maneno ya Kashfa na Kebehi, wanatakiwa kupuuzwa kwa hali zote, kwani Simba SC ina mipango yake kuelekea msimu ujao, baada ya kuanguka msimu huu.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe huo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kwa kuandika: Nipo imara na naendelea na mapambano

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA IKIPITIA KIPINDI KIGUMU KWENYE LIGI...MZEE DALALI AIBUKA NA HILI...AMTAJA BARBARA NA TRY AGAIN..