Home Habari za michezo KISA ‘MGOLI WA KIBABE’ WA FEI TOTO DHIDI YA SIMBA….SHABIKI YANGA AFARIKI...

KISA ‘MGOLI WA KIBABE’ WA FEI TOTO DHIDI YA SIMBA….SHABIKI YANGA AFARIKI KWA KUZIDIWA NA FURAHA….


Imekuwa ni wakati wa simanzi na vilio kwa familia ya James Mhamba (60) ambaye alikuwa shabiki wa Timu ya Yanga na mkazi wa Rwamishenye katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambaye amepoteza maisha baada ya mechi ya kumalizika kati ya Yanga vs Simba huku chanzo cha kifo chake kikidaiwa kuwa ni furaha iliyopitiliza kufuatia timu yake kuibuka na ushindi.

Mechi hiyo iliyochezwa juzi Jumamosi, Mei 28, 2022 katika Dimba la CCM Kirumba Mwanza ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kuipeleka Yanga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Wakizungumzia tukio hilo, majirani na marafiki wa mzee Mhamba wanasema;

“Mzee mhamba alikuwa kiongozi kwenye umoja wetu wa Simba na Yanga (YASI), alikuwa shabiki mzuri wa Yanga, ni mtu aliyekuwa amehamasika na timu yake. Yanga ikishindwa alikuwa ananyong’onyea lakini ikishinda anachangamka sana.

Mimi nilionana naye jana kabla ya mechi alikuwa mzima tu, lakini leo nikapigiwa simu kuwa amekufa sikuamini kabisa, nimefika hapa nyumbani nikakuta kweli ameshafariki, basi tukafanya taratibu za kuupeleka mwili mochwari. Inasikitisha sana.

Alikuwa mcheshi sana na Sahabiki kindakindaki wa Yanga, ana rekodi za Yanga atakutajia wachezaji na rekodi za timu yake, sio shabiki lakini mpira alikuwa anaufahamu. Ilikuwa lazima avae jezi ya yanga, hivyo unaweza kuona alivyoipenda timu yake,” Hamidu Abdinul, mkazi wa eneo hilo.

Alikuwa na maradhi ya presha, baada ya mchezo wa jana (yaani juzi kati ya Simba vs Yanga), furaha ilizidi, huenda presha ilipanda ikasababisha kifo chake, amekuwa akinifundisha mengi ya kiuongozi katika chama chetu hiki, nilionana nae jana wakati wa mechi yeye akawa anaangalia kwake mimi nikaenda sehemu nyingine.

Wanasema baada ya mechi kumalizika, alitoka eneo alilokuwa akiangalia akaingia ndani, akavua shati lake akidai kuwa anahisi joto kali, alikwenda kwenye bomba kujimwagia maji ya baridi, hapo hapo ndipo alianguka chini.

“Wakaita majirani akiwemo mzee Denis, lakini walipokuwa wakimuingiza ndani aliwaambia wamfunike, watoto wake wakakataa wakisema wampeleke Hospitali, Mzee Denis ilibidi awaambie ukweli kwamba tayari ameshafariki dunia,” amesema Katibu wa chama cha Yanga na Simba (YASI).

SOMA NA HII  HII HAPA 5 HOT STRIKE YA MERIDIANBET CASINO...HAPA MKWANJA NI UHAKIKA...