Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKILIA NA MAJERAHA KWA WACHEZAJI WAO…YANGA SIRI IKO HIVI…

WAKATI SIMBA WAKILIA NA MAJERAHA KWA WACHEZAJI WAO…YANGA SIRI IKO HIVI…

Kikosi cha Yanga SC

Kocha wa viungo wa Yanga, Helmy Gueldish amefichua siri ya ubora wa mastaa wa timu hiyo ni kuzingatia mazoezi ambayo yamekuwa yakiwaepusha na majeraha ya mara kwa mara na kudai wapinzani wao katika Ligi Kuu, Kombe la ASFC na hata Kombe la Shirikisho Afrika kazi wanayo.

Gueldish alitua Yanga akitokea klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia ikiwa ni pendekezo la kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi, aliyekuwa amebaini nyota wake kutokuwa na mwendelezo mzuri katika kipindi cha pili mwanzoni alipotua klabuni hapo.

Akizungumza Helmy alisema pamoja na ratiba ngumu waliyonayo mastaa wake anafurahi wamemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa na idadi ndogo ya majeruhi huku akikiri hiyo inatokana na kuzingatia kwa mpangilia wa mazoezi.

“Yanga kila mara baada ya mchezo wamekuwa fakifanya mazoezi mepesi ya kuweka mwili sawa na baada ya hapo siku inayofuata wanaingia ‘GYM’ kuweka miili sawa hii inasaidia sana kuwafanya wachezaji wajisikie vizuri na kuiweka sawa miili yao,” alisema kocha huyo Mtunisia kipenzi cha mashabiki wa Yanga hasa kwa staili yake ya kushangilia mabao kwa midadi mingi, aliyeongeza;

“Mbali na hilo pia wana utaratibu wa kuingia kwenye maji yenye mabarafu ambayo kwa umri wao yanasaidia kuwarudisha mwili kwenye utimamu wake hii inasaidia sana kupunguza uchovu ambao wachezaji wengi wamekuwa wakiupitia kutokana na ratiba ngumu ya ligi.”

Alisema mazoezi ya kuingia kwenye mabarafu yanaumiza na wachezaji wengi huwa wqanayakimbia lakini yanasaidia sana kurudisha miili yao kwenye hari ya kawaida amelisimamia hilo kwa upande wa Yanga na ndio maana timu imeweza kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na idadi ndogo ya majeruhi.

Helmy alitumia nafasi hiyo pia kumpongeza Nabi kwa kutumia wachezaji kwa kufanya mabadiliko ya mara kwa mara ili kutoa nafasi ya kupumzisha miili ya baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakitumika mara kwa mara.

“Kitendo cha kusajili idadi kubwa ya wachezaji pia ni moja ya faida iliyochangia mastaa wengi wa timu yetu ambao wamekuwa na hari ya upambanaji kutokupata majeraha ya mara kwa marea kwani kocha amekuwa akifanya mabadiliko ya kutoa nafasi ya kila mchezaji kupata nafasi ya kucheza,” alisema na kuongeza;

“Duru la pili utakuwa mgumu na wenye ushindani wachezaji watatumika sana hili nalifahamu na nimeandaa programu maalum ambayo itaendelea kuwaweka kwenye hari nzuri ingawa majeraha huwa yanatokea kama ilivyo kwa Abutwarib Mshery, Heritier Makambo ambao watakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.”

Mbali na ubora wa Gueldish katika mazoezi ya viungo, pia anajua kuchambua ubora wa wapinzani kazi ambayo anaifanya kuelekea kila mchezo.

SOMA NA HII  ALLY KAMWE AFUNGUKA HISTORIA HII MBAYA KWA YANGA