Home news GOMES AFUNGUKA MENGINE KUHUSU SIMBA…AGUSIA KIKOSI..AMTAJA CHAMA NA LUIS MIQUISSONE..

GOMES AFUNGUKA MENGINE KUHUSU SIMBA…AGUSIA KIKOSI..AMTAJA CHAMA NA LUIS MIQUISSONE..


ALIYEKUWA kocha mkuu wa Simba, Diddie Gomes amesema pamoja na timu hiyo kuondolewa katika hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika anaiona mbali Shirikisho.

Simba wameondolewa na Jwaneng Galaxy baada ya kukubali kipigo cha bao 3-1 nyumbani wakati mchezo wa kwanza walipata ushindi wa bao 2-0 ugenini.

Amesema Simba imeshindwa kufanya vizuri kwenye hatua hiyo kutokana na kuwa na nyota wengi wageni kikosini huku akiwataja Luis Miquissone na Clatous Chama kuwa wamechangia kuondolewa kwao.

“Simba ni timu mpya inahitaji muda kuwa bora pamoja na yote imeanza vibaya kutokana na kupata majeraha kwa nyota wao ambao pia ni muhimu kikosini,” anasema na kuongeza kuwa;

“Chama na Luis walikuwa na mchango mkubwa kikosini walikuwa wanatengeneza na kufunga ni jambo la muda kupata nyota kama hao kwa haraka kikosini,” anasema.

Gomes amesema muda ambao Simba wanacheza na Red Arrows nyota wengi watakuwa wamepata muunganiko na timu sambamba na kurudi kwenye hari zao za kawaida baada ya majeruhi waliyoyapata.

SOMA NA HII  KUBEZA KILICHOFANYWA NA SIMBA KINSHASA NI KUJITENGENEZEA UGUMU WA MABADILIKO YA FIKRA….