Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA ATOA KAULI YA KISHUJAA, WAAMUZI WATAJWA

MBELGIJI WA SIMBA ATOA KAULI YA KISHUJAA, WAAMUZI WATAJWA

KUELEKEA kwenye mechi ya kesho kati ya Mtibwa Sugar na Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba ametoa kauli ya kishujaa kwa mashabiki na viongozi.

Sven anakumbukumbu ya kupoteza mchezo wake uliopita Uwanja wa Uhuru kwa kuchapwa bao 1-0 na JKT amesema kuwa kesho hakutakuwa na sababu ya kutaja zaidi ya ushindi kwa timu yake.

“Hakuna sababu iwe ni hali ya uwanja, mvua, jua au waamuzi wa mchezo kesho haipaswi kuwa sababu. Ni ushindi pekee ndio tunahitaji na tuna kazi ya kuhakikisha tunafanikisha hilo.”.

Kwenye jumla ya mechi 10 ambazo amekaa benchi akiwa ni Kocha Mkuu baada ya kupokea mikoba ya Patrick Aussems amepoteza mchezo mmoja na kulazimisha sare moja huku akishinda mechi nane za ligi.

SOMA NA HII  JKT TANZANIA V SIMBA MATOKEO YAO YA MECHI ZAO HAYA HAPA