Home Habari za michezo SIMBA WATIA MKONO KWENYE MCHEZO WA ‘BASKETBALL’…JAMBO LAO HILI HAPA…

SIMBA WATIA MKONO KWENYE MCHEZO WA ‘BASKETBALL’…JAMBO LAO HILI HAPA…

Simba SC

Uongozi wa Klabu ya Simba, umeruhusu Daktari wa timu ya wanawake (Simba Queens), Lanina Munisi kwenda kutoa huduma ya kitabibu kwenye timu ya mpira wa kikapu ya Pazi.

Pazi inajiandaa na mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Ligi ya Mabingwa kwa mchezo huo Afrika (BAL) ambayo yanatarajia kuanza wiki ijayo Afrika Kusini ikiwa ni hatua ya pili .

Pazi ndio mwakilisha wa nchi kwenye michuano hiyo mikubwa ya kikapu ambapo ilifuzu hatua ya kwanza mashindano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni

Pazi ipo kundi moja na wenyeji Cape Town Tiger, Dynamos, Junior NBA Academy. Mshindi wa kundi hilo ndiye ataingia hatua ya fainali zitakazochezwa Senegal,.

Mwenyekiti wa Pazi, Ladislaus Ikungura amesema kuwa timu yao haikuwa na daktari na mashindano hayo makubwa ni lazima kila timu iwe na daktari mwenye sifa zote ndipo walipowaomba Simba na kumruhusu Daktari wao.

“Kiukweli tunawashukuru sana Simba kutupatia daktari wao, haya ni mashindano makubwa ambayo yanatakiwa kufuata kanuni zote pasipo kuvunja, hivyo tutoe shukrani kwa viongozi wa Simba na wale wote wanaotusapoti kwenye safari hii.

“Hii ni mara yetu ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa, hivyo tunaenda kama timu changa, mambo mengi ni mageni ila naamini tutafanya vizuri, timu inatarajia kuondoka usiku wa kuamkia Jumapili na ratiba yetu ya kucheza itaanza Jumanne (Novemba 28, 2023) dhidi ya Dynamo,” amesema Ikungura

Naye Lanina amesema; “Hii ni kazi yangu, nipo hapa kwa muda na ninaushukuru uongozi wangu kuniruhusu kufanyakazi na Pazi, bado ni mfanyakazi wa Simba hivyo mashindano haya yakimalizika nitarudi kwenye majukumu yangu ya Simba Queens ingawa hata sasa huwa naenda mazoezini tukimaliza ndio nakuja huku.”

SOMA NA HII  MSAUZI KUPEWA U-CEO SIMBA....KAJULA AANZA KUAGA WACHEZAJI....ISHU NZIMA IKO HIVI...