Habari za michezo

KUELEKEA MECHI NA SIMBA LEO…MKWASA KAJIPIGA PIGA KIFUANI NA KUTOA KAULI HII YA KIBABE AISEE…

admin May 8, 2022 1:05 pm


KOCHA wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akiwaambia wasiogope, kwani anaamini nidhamu itawapa pointi tatu leo dhidi ya Simba wa Ligi Kuu Bara.

Mkwasa alisema mchezo uliopita na Yanga ulioisha kwa suluhu uliwapa morali wachezaji na leo watashuka ili kukamilisha jambo lao katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tunaenda katika mchezo huu kwa tahadhari kubwa kama tulivyocheza na Yanga, ni mechi ngumu hivyo ili kupata kile tunachokikusudia yatupaswa kujiandaa kimwili na kiakili,” alisema.

Hii ni mara ya tatu kwa timu hizo kukutana msimu huu baada ya awali Ruvu kufungwa 3-1 na Simba katika mechi ya kwanza wa Ligi uliopigwa jijini Mwanza kisha kuchapwa mabao 7-0 katika ASFC raundi ya 16 Bora, Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam.

KUELEKEA MSIMU UJOA…MAKUMBI AIPA YANGA MAJEMBE YA KAZI…HAO MASTRAIKA NI VIFAA HASWA… FEI TOTO AFUNGUKA YAKE NA YANGA….ADAI IWE ISIWE LAZIMA KIELEWEKE…AGUSIA ALIVYOVUMILIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply