Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA LEO….DODOMA JIJI WAMWANDALIA MAYELE ‘KAZI CHAFU’ …WACHEZAJI WALA KIAPO…

admin May 15, 2022 2:06 am


Kocha Msaidizi wa Kikosi cha Dodoma Jiji Mohammed Muya amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Yanga huku akidai wamejipanga kuhakikisha mshambuliji wa Yanga Fiston Mayele hatetemi.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi kuu ikiwa na alama 28 huku vinara Yanga wakiwa kileleni na pointi 57.

Kocha huyo amesema: “Hiyo kutetema kwetu hatuifikirii kabisa nimekwambia sisi niwahitaji kutetema hakupo kesho ‘leo’,”

Amesema morali ya wachezaji ipo juu na michezo yao mitatu ya mwisho wamepata alama saba wakishinda dhidi ya Biashara, Mbeya City na kutoka suluhu dhidi ya Polisi Tanzania ugenini.

“Kama mwalimu unajua kinachotakiwa kwa wachezaji wako hakuna cha kuogopa timu yoyote, vigezo vya kuwa washindani tunavyo tunawaita mashabiki wetu waje.

Mchezaji wa timu hiyo,Omary Kanyoro amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

MORRISON AIBUA MAPYA SIMBA…ABEBA KILA KITU KAMBINI…AZIZI KI AJIPELEKA MSIMBAZI…MOSES PHIRI KUTUA… ENDAPO LIKATOKEA LA KUTOKEA LEO DHIDI YA DODOMA….NADI AWAWAHI YANGA…ATOA SABABU MAPEMAAA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply