Home Azam FC KWA MWENDO HUU..EBU TUAMBIZANE UKWELI WANANZENGO…SHIDA YA AZAM NI KOCHA AU KUNA...

KWA MWENDO HUU..EBU TUAMBIZANE UKWELI WANANZENGO…SHIDA YA AZAM NI KOCHA AU KUNA JINGINE…?


Azam FC msimu huu inahitaji maombi. Inapitia katika nyakati ngumu kuliko wakati mwingine wowote. Inaumiza sana. Nani aliwahi kuwaza Azam itafika wakati hadi nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu wanaitafuta kwa tochi? Hilo jambo limetokea msimu huu.

Azam ipo ovyo kwelikweli. Kipigo dhidi ya Kagera Sugar wiki hii ulikuwa kama msumari wa moto katikati ya kidonda kibichi. Kilikuwa ni kipigo cha nne katika mechi saba za mwisho.

Katika mechi hizo Azam imeshinda moja na sare mbili. Yaani imepata alama tano tu kati ya 21. Ni ajabu na kweli.

Kila mtu aliamini tatizo la Azam msimu huu ilikuwa mbinu mbovu za George Lwandamina. Wakafumba macho na kumfurusha kabla mambo hayajawa magumu. Nini kimebadilika? Hakuna. Azam imezidi kuwa hoi zaidi. Yaani baada ya mechi 21 (kabla ya jana usiku dhidi ya KMC) Azam ipo nafasi ya nne na alama 29. Ni alama nane tu tofauti na Coastal Union iliyopo mkiani mwa Ligi.

Imeachwa alama 27 na vinara Yanga. Hii ndio iliyokuwa ikigombea ubingwa miaka mitano nyuma. Azam ilishindana vilivyo na ile Yanga ya Manji. Haikukubali unyonge hata kidogo.

Ajabu ni kwamba msimu huu Azam inashindana na Namungo, KMC na Polisi Tanzania. Simba na Yanga siyo washindani wake tena. Je tatizo la Azam FC ni kocha? Huyu Abdihamid Moallin si alianza na moto? Kila mtu akakubali kuwa ni kocha bora.

Nini kimemkuta? Nadhani Azam ina tatizo kubwa zaidi ya kocha. Kama haitalitatua shida itaendelea kuwepo kwa miaka mingi zaidi.

SOMA NA HII  SHABIKI WA YANGA ALIYEPOKEA KIPIGO NA MASHABIKI WA SIMBA AFUNGUKA TUKIO ZIMA HAPA