Home Habari za michezo MIAKA KUMI YA KIFO CHA MAFISANGO..HIZI HAPA PANDA SHUKA ZA SIMBA SC…WALIPITIA...

MIAKA KUMI YA KIFO CHA MAFISANGO..HIZI HAPA PANDA SHUKA ZA SIMBA SC…WALIPITIA UKAME NA SHIDA ZA AJABU….


Siku kama ya jana  miaka 10 iliyopita, mchezo wa soka nchini ulimpoteza mmoja wa viungo bora, Patrick Mutesa Mafiosango ambaye hadi anafikwa na umauti alikuwa akiitumikia Simba na timu ya taifa ya Rwanda.

Marehemu Mafisango alifariki Mei 17, 2012 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Keko, Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2011/2012 ambao Simba walitwaa ubingwa.

Hadi wakati mauti yanamfika, Mafisango alikuwa na umri wa miaka 32 na kabla ya kuitumikia Simba aliwahi kuchezea timu za TP Mazembe, APR, Atraco na Azam.

Baada ya kifo cha Mafisango, Simba imepita katika nyakati za furaha lakini pia yapo magumu ambayo klabu hiyo imepitia.

Haya ni baadhi ya mambo yaliyotokea Simba katika kipindi cha miaka tisa bila Mafisango.

Ukame wa misimu mitano

Mara baada ya Simba kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2011/2012, ilipita kipindi cha misimu mitano mfululizo bila kutwaa taji la Ligi Kuu

Lakini pia baada ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2013 na kutolewa katika hatua ya awali na timu ya Recreativo do Libolo ya Angola, hawakushiriki tena mashindano ya klabu Afrika hadi mwaka 2018 waliposhiriki Kombe la Shirikisho Afrika

Mataji 15

Katika kipindi cha miaka tisa ambacho kimepita bila Mafisango kuwepo katika uso wa dunia, Simba imetwaa jumla ya mataji 14 katika mashindano tofauti iliyoshiriki.

Imetwaa mataji manne ya Ligi Kuu, matatu ya Kombe la Shirikisho la Azam, Mtani Jembe (2), Ngao ya Jamii (5), Mapinduzi (2) na taji moja la Simba Super Cup

Jeuri Afrika

Tangu Marehemu Mfisango alipofariki hadi sasa, Simba ndio timu iliyofanikiwa zaidi kimataifa kuliko nyingine yoyote hapa nchini.

Simba imeshiriki mashindano ya kimataifa mara nne na kati ya hizo nne, mara mbili imetinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kagere amlindia heshima

Ni Wanyarwanda wawili ambao wameichezea Simba tangu Mafisango alipofariki ambao ni Haruna Niyonzima aliyesajiliwa kutoka Yanga na Medie Kagere aliyenaswa na Simba kutokea Gor Mahia.

SOMA NA HII  GOAL LA LUIS MIQUISSONE LAMFANYA RAIS WA AL AHLY KUCHUKUA UAMUZI HUU..!!

Niyonzima hakuwa na nyakati nzuri ndani ya Simba lakini Kagere ameonekana kuwapooza mashabiki wa timu hiyo machungu ya kumkosa Mafisango kwani katika misimu mitatu aliyoichezea amegeuka mwiba katika kufumania nyavu za timu pinzani na ushahidi wa hilo, mshambuliaji huyo wa Rwanda amefunga jumla ya mabao 63 katika Ligi Kuu ndani ya misimu minne aliyoichezea timu hiyo.

Simba Queens yaibuka, yatwaa mataji

Hadi wakati Mafisango anafariki, Simba haikuwa na timu ya wanawake lakini mwaka 2016, lianzishwa na kupewa jina la Simba Queens na hadi sasa imeshatwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here