Habari za michezo

MORRISON AIBUA JIPYA AKIWAGA WENZAKE KAMBINI…KAKUSANYA MPAKA MASHUKA…MZAMIRU AMTUPA YANGA…

admin May 15, 2022 11:31 am


KUFUATIA taarifa ya kupewa mapumziko mpaka mwishoni mwa msimu huu, kiungo mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ameibua mapya kikosini hapo.

Morrison ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwisho wa msimu huu, alijiunga na timu hiyo msimu wa 2020/21 baada ya kuondoka Yanga.

Juzi Ijumaa baada ya kupewa likizo hiyo, aliwaaga wenzake kambini huku akiwataka kuhakikisha wanapambana kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu.

Morrison alisema: “Niko hapa kwa dhumuni moja kubwa la kurejesha shukrani zangu za dhati kwenu nyote katika kipindi ambacho nimekuwa mchezaji wa Simba.

“Licha ya kwamba mimi bado ni mchezaji wa Simba kimkataba, lakini kwa manufaa mapana ya klabu hii na mimi binafsi, sitaendelea kuwa na timu mpaka mwishoni mwa msimu.

“Sina tatizo lolote na uongozi na nawatakia kila la kheri mpaka pale tutakapokutana tena.”

Morrison wakati anaondoka kambini, alionekana akiwa ameshika blanketi lake na mabegi ikionesha kwamba amebeba kila kilicho chake, huku kiungo wa timu hiyo, Mzamiru Yassin akimtania kuwa anaenda Yanga.

KUELEKEA MSIMU UJAO….SIMBA KUSHUSHA ‘KIFAA HIKI CHA KINIGERIA’….ANAKIPIGA LIGI YA URENO…ISHU IKO HIVI… DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA DODOMA…SURE BOY LAMKUTA JAMBO YANGA…KAZE AJIPIGA KIFUA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply