Home Habari za michezo ‘MTAMBO WA KUFUNGA MAGOLI’ ULIOTIKISA AFCON MBIONI KUTUA YANGA…AGANA NA TIMU YAKE...

‘MTAMBO WA KUFUNGA MAGOLI’ ULIOTIKISA AFCON MBIONI KUTUA YANGA…AGANA NA TIMU YAKE YA SAUZI…


KIUNGO mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Gabadinho Mhango ameweka wazi kuwa anatarajia kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu ambapo hiyo ni habari nzuri kwa Yanga ambao wamekuwa wakimuwinda kwa nguvu.

Winga huyo ambaye alimtungua kipa wa Simba, Aishi Manula kwa penalti kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika amekuwa akifatiliwa kwa ukaribu na Yanga ambao tayari wameshaanza harakati za kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao wakiwa wanataka kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa.

Akizungumza, Gabadinho ambaye ni raia wa Malawi amesema kuwa, msimu utakapomalizika hatakuwa na uhakika wa kusalia Orlando huku akiwa na uhakika wa kuwa katika timu mpya.

SOMA NA HII  KIMENUKAAH...CAF WAANZA KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WASAUZI KUHUSU VAR KUZIMWA KWA MKAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here