Home Habari za michezo PAMOJA NA WOTE KUWA WAFUNGAJI HATARI….MPOLE ATABIRIWA MAKUBWA ZAIDI KULIKO MAYELE…

PAMOJA NA WOTE KUWA WAFUNGAJI HATARI….MPOLE ATABIRIWA MAKUBWA ZAIDI KULIKO MAYELE…


Kocha wa Geita Gold FC, Fred Felix Minziro ameibuka na kusema kuwa Mshambuliaji wa klabu hiyo George Mpole ana nafasi kubwa ya kuwa Mfungaji Bora msimu huu mbele ya Fiston Mayele wa Young Africans.

Mpole kwa sasa anafukuzana na Fiston Mayele katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora, akiwa ameshafunga mabao 11, huku mpinzani wake akiwa na mabao 13.

Minziro anaamini Mpole ana nafasi kubwa ya kufunga zaidi katika michezo iliyosalia kwa msimu huu na kumpita Mayele na mwisho wa msimu kuwa mfungaji bora.

“Hakuna ugumu kwa Mpole kufikisha idadi kubwa ya mabao msimu huu kutokana na maarifa na jitihada anazozionyesha.”

“Muda wote akiwa uwanjani anafikiria kufunga kama alivyo Mayele na kimsingi ni ngumu kuwatofautisha washambuliaji hawa kwa muda huu kwani wanapokuwa uwanjani muda wowote unaweza kuona wakifunga na ndio maana namuona Mpole akifanya makubwa zaidi.” amesema Minziro

Huu ni msimu wa kwanza kwa George Mpole kucheza Ligi Kuu akiwa na klabu ya Geita Gold FC kama ilivyo kwa Mayele aliyesajiliwa Young Africans akitokea AS Vita ya kwao DR Congo.

SOMA NA HII  KISA KUTOKUONDOKA NCHINI KAMA ALIVYOOMBA...KIGOGO SIMBA AMLIPUA MORRISON....ADAI SIMU HAPOKEI...AITAJA YANGA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here