Home Habari za michezo WAKATI MAN UNITED WAKIMUONA POGBA KAMA ‘MUIGIZAJI ZAIDI’ ….MAN CITY WAMNYATIA KIMYA...

WAKATI MAN UNITED WAKIMUONA POGBA KAMA ‘MUIGIZAJI ZAIDI’ ….MAN CITY WAMNYATIA KIMYA KIMYA…

 


Manchester City inaweza kufanya usajili wa kushtukiza wa kiungo Paul Pogba ambaye Mkataba wake na Manchester United unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Pep Guardiola anafikiria kumsajili Pogba ambaye atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu na lengo kubwa ni kuziba nafasi ya kiungo mkabaji itakayoachwa na Fernandinho ambaye ameamua kuondoka katika Klabu ya Manchester City.

Manchester City imejiondoa rasmi kwenye mbio za kuwania saini ya Declan Rice wa West Ham United ambaye thamani yake ni Paundi Milioni 100 hivyo The Citizen huenda wakatumia nafasi hiyo kumsaidi Pogba ambaye hatowagharimu ada ya uhamisho.

Hali ya Pogba imekuwa matatani kufuatia kifo cha wakala wake Mino Raiola ambaye ndiye aliyekuwa akishughulikia masuala yake ya usajili.

Iwapo Pogba atajiunga na Manchester City itakuwa ni tukio litakaloshabihiana na lile la Carlos Tevez ambaye mnamo mwaka 2009 alikataa ofa ya The Red Devils ya kuwatumikia kwa mkataba wa kudumu baada ya ule wa mkopo kumalizika na kisha kuamua kutimkia kwa Man City.

Tangu arejee kwa mara ya pili ndani ya Man United mwaka 2016 kwa ada ya uhamisho iliyoweka rekodi EPL, Pogba ameichezea Red Devils jumla ya michezo 154 na kuifungia mabao 29.

SOMA NA HII  MCHAGA WA KILUVYA ALIYESHINDA JACKPOT YA SportPesa.. AKABIDHIWA UBILIONEA WAKE LEO....AFUNGUKA ALICHOFANYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here