Home Habari za michezo YANGA WAFANYA KUFRU MKATABA MPYA WA MWAMNYETO…APEWA MIAKA MIWILI YENYE MAMILIONI YA...

YANGA WAFANYA KUFRU MKATABA MPYA WA MWAMNYETO…APEWA MIAKA MIWILI YENYE MAMILIONI YA PESA…


NAHODHA na beki wa kati tegemeo ndani ya Yanga, Bakari Mwamnyeto, ameongeza mkataba wa miaka miwili wenye thamani inayotajwa kufikia shilingi milioni 200 kuendelea kukipiga Jangwani.

Beki huyo ameongeza mkataba kuendelea kuichezea timu hiyo, baada ya ule wa awali wa miaka miwili kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mwamnyeto ni kati ya mabeki waliokuwa wakitajwa kuwaniwa na Simba kuelekea msimu ujao kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu kikosini hapo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikaa, beki huyo amekubali kuongeza mkataba baada ya makubaliano ya pande mbili kufikia muafaka.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, beki huyo alisani mkataba huo siku chache kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba uliochezwa wikiendi iliyopita.

“Yanga hii hakuna mchezaji atakayeondoka kwa wale ambao tunawahitaji kwa ajili ya msimu ujao. Wote wanabaki.

“Uongozi upo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji wetu ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na kati ya hao alikuwepo Mwamnyeto.

“Tayari Mwamnyeto ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga wenye thamani ya Sh 200Mil,” alisema mtoa taari

Yanga kupitia Mjumbe wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alisema kuwa: “Hakuna mchezaji atakayeondoka Yanga ambaye bado anahitajika.

“Hizo tetesi mnazozisikia za wachezaji kuondoka mwishoni mwa msimu akiwemo Mwamnyeto si za kweli, ataendelea kubaki hapa.”

SOMA NA HII  JINA LA KINDA WA AZAM FC, TEPSI EVANCE LATAJWA TENA ...KOCHA ULAYA APAGAWA BAADA YA KUONA VIDEO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here