Habari za Simba SC
Habari za michezo

KWA MOTO HUU WA JOHN BOCCO….MBEYA CITY WATAFUTE PA KUKIMBILA LEO…KAMA SIO 2 NI 3…

admin January 18, 2023 6:45 pm

Wakati Simba wakijiandaa kuwavaa Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Januari 18, Simba bado wanajivunia kiwango cha Nahodha wao John Bocco anaerudisha makali yake katika safu ya ushambuliaji msimu huu.

Mabao 9 aliyofunga John Raphael Bocco katika NBC Primia Lig msimu huu hadi sasa, ameyafunga katika michezo mitano tofauti.

ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao zaidi ya nane katika michezo michache tofauti kwenye NBC Primia Ligi msimu huu.

dhidi ya Ruvu Shooting (mabao 3)

dhidi ya Tanzania Prisons (mabao 3)

dhidi ya Polisi Tanzania (bao 1)

dhidi ya Geita Gold (bao 1)

dhidi ya Kmc (bao 1)

Takwimu za John Bocco kwenye NBC Primia Ligi msimu huu hadi sasa

michezo 11

dakika alizocheza 815

mabao 9

pasi ya bao 1

amehusika katika mabao 10

ana wastani wa kufunga bao kila baada ya dakika 90

atakuwa kibaruani dhidi ya Mbeya City leo, amefunga manne katika michezo mitano iliyopita ya ligi dhidi yao.

WEWE SHABIKI WA SIMBA AU YANGA….CHUKUA HII ITAKUSAIDIA KUTAMBA MTAANI KIBABE… HIVI HAPA SABABU ZA NDAANI MASTAA HAWA KUKOSEKANIKA SIMBA LEO…JAMBO HALIJASEMWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply