Habari za Simba
Habari za michezo

HIVI HAPA SABABU ZA NDAANI MASTAA HAWA KUKOSEKANIKA SIMBA LEO…JAMBO HALIJASEMWA…

admin January 18, 2023 6:48 pm

Wachezaji Peter Banda, Henock Inonga, Israel Mwenda na Mosses Phiri hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kitakachoshuka Dimbani leo Jumatano (Januari 18).

Simba SC itakua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuikabili Mbeya City FC, katika mchezo wa Mzunguuko wa 20 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao rasmi utaanza saa moja usiku.

Taarifa kutoka Simba SC imeeleza kuwa Wachezaji hao wanne hawana utimamu wa mwili, baada ya kuuguza majeraha.

Wakati huohuo Simba SC imepangwa kuutumia mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kupitia Dirisha Dogo, kwa Mashabiki wake watakaojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji hao ni Mshambuliaji Jean Baleke (DR Congo), Kiungo Ismael Sawadogo (Burkina Faso) na Mshambuliaji Mohamed Mussa (Tanzania).

KWA MOTO HUU WA JOHN BOCCO….MBEYA CITY WATAFUTE PA KUKIMBILA LEO…KAMA SIO 2 NI 3… FT: SIMBA 3-2 MBEYA CITY….NTIBAZONKIZA AENDELEA KUWAPA MAWAZO YANGA…CHAMA MHH…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply