Habari za michezo

EDO KUMWEMBE: VIONGOZI SIMBA SC WANAPAMBANA KUIVUNJA TIMU YAO…WANATAKA IONEKANE KAMA PRISONS TU….

admin June 1, 2022 2:18 am


Mwandishi wa Habari za Michezo Mwandamizi Edo Kumwembe amewashangaa baadhi ya Viongozi wa zamani wa Simba SC ambao wanapambana kuwaaminisha Mashabiki na Wanachama kuwa timu yao ni mbovu.

Simba SC imepoteza mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, na itamaliza msimu huu ikiwa na taji la Mapinduzi pekee.

Kumwembe ambaye pia ni Mchambuzi wa Michezo wa Kituo cha Wasafi Media amesema anaashangazwa kuona baadhi ya viongozi wa zamani wa klabu hiyo wakitumia nafasi ya kushindwa kutwaa mataji kwa kigezo kisichokua na mantiki.

Amesema Simba SC haijafanya vibaya kama inavyoelezwa na Viongozi hao wa zamani, zaidi ya kutafuta sababu za kuwaaminisha watu kwa kuifananisha klabu hiyo kama Tanzania Prisons ambayo haina matokeo mazuri msimu huu.

“Vile naangalia baadhi ya Viongozi wa zamani wa Simba wakipambana kuivunja timu yao wanahaha kweli kweli nilidhani katiba mpya walio ipitisha itaondoa haya mambo, Aah wapi.

“Simba wanamaliza wa pili katika ligi, robo fainali katika Shirikisho barani Afrika na nusu fainali katika FA. Lakini watu wanataka ionekane imefanya vibaya kama Prisons tu.” amesema Kumwembe

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Kassim Dewji na Mjumbe wa Bodi Mwina Kaduguda ni sehemu ya viongozi ambao wameonesha kuwa tofauti na kinachoendelea Simba SC.

AMAZULU YA AFRIKA KUSINI WAMPA OFA NONO PABLO…KULIPWA MILIONI 77 KWA MWEZI…ORLANDO NA RAJA NAZO ZAMTAKA… BAADA YA PABLO…FAGIO ZITO KUPITA NA HAWA SIMBA…KOCHA MSAUZI NAYE YAMKUTA…YANGA WATEGUA MTEGO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply