Habari za michezo

BAADA YA KUMALIZANA NA WATATU CHAP….YANGA WAPANGA KUWAFANYIA ‘UNYAMBISI’ MASTAA WAKE WALIOBAKI…

admin June 4, 2022 2:49 am


Hadi sasa Yanga imemalizana na mastaa watatu tu kati ya 10 wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu.

Wachezaji waliopata mikataba ni pamoja na nahodha Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari na Zawadi Mauya huku wengine saba wakiwa bado hawajaongezewa mikataba.

Waliobaki ni Farid Mussa, Yassin Mustafa, Abdallah Shaib ‘Ninja’, Balama Mapinduzi, Yacouba na Said Ntibazonkiza (mkono wa baibai) Deus Kaseke na Paul Godfrey inasemekana wamemalizana na Singida Big Boy.

Chanzo hicho, kilisema ambao bado hawajaongezwa mikabata watasainishwa bila dau la usajili zaidi ya kuwaongezea token kwenye mishahara. Yanga wamekuwa wakifanya mambo yao ya usajili kimyakimya kwa madai kwamba wanataka kukamilisha orodha yao kwanza kwani misimu ya hivikaribuni walipigwa tikitaka zisizo na maana yoyote.

SIKU CHACHE BAADA YA PABLO KUTIMULIWA…SIMBA WAANIKA IDADI YA MAKOCHA WALIOTUMA MAOMBI YA KAZI… SAMATTA: NI BAHATI MBAYA TUNAANZIA UGENINI…NIGER NAO WANAITAMAN AFCON KAMA SISI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply