Habari za michezo

BINGWA NBC PREMIER LEAGUE KULAMBA MILIONI 600…KOMBE JIPYA LATAMBULISHWA…YANGA WATAKAA NALO SIKU 30 TU…

admin June 9, 2022 11:27 am


Bodi ya Ligi imetaja kitita cha Sh 1.8 Bilioni kama zawadi na bonusi kwenye Ligi msimu huu huku bingwa akitengewa Sh 100 milioni kutoka NBC na Sh 500 Milioni kutoka Azam.

Ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kassongo amebainisha hayo leo wakati wa kutambulisha kombe atakalokabidhiwa bingwa wa msimu huu.

Amesema mshindi wa pili ataondoka na Sh50 milioni kutoka NBC na Sh250 milioni kutoka Azam.

“Watatu atazawadiwa Sh30 milioni kutoka kwa mdhamini wa Ligi, lakini pia 225 kutoka Azam,” amesema.

Katika zawadi hizo, NBC imetenga Sh20 milioni kwenye zawadi ya timu yenye nidhamu.

Kuhusu kombe, Kassongo amesema muonekano wa kombe la ligi utakuwa wa kombe lililotambulishwa leo hadi pale itakavyoamuliwa vinginevyo.

“Bingwa atakaa nalo mwezi mmoja na kulirejesha endapo atalitetea mara tatu ndipo atalichukua moja kwa moja,”

KISA CAF…IBENGE, MOSIMANE WARUDI RASMI DARASANI UPYAA….KOCHA WA MANE NAYE NDANI…THIERRY HENRY APEWA SHAVU… KUELEKEA MSIMU UJAO…TRY AGAIN AIBUKA NA MPANGO WA KUISUKA UPYA SIMBA…MAJEMBE MAPYA KUANZA KUSAINI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply