Habari za michezo

NJAA YAIFANYA NDANDA FC KUWA KAMA CHELSEA AISEE…MABOSI WAAMUA KUIUZA BILA MASHARTI MENGI…

admin June 14, 2022 4:23 pm


Ndanda Fc maarufu ya mkoani Mtwara ambayo inashiriki ligi kuu daraja la kwanza inauzwa rasmi kutokana na kukosa fedha za kujiendesha.

Mkurugenzi wa Bodi ya timu hiyo, Said Limbega amesema uongozi umeridhia kuiuza kwa kuwa imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo uwezo wa kifedha, kwani timu hiyo inapitia kipindi kigumu katika kushiriki kwenye mashindano.

Amesema timu, maarufu Wanakuchele inauzwa bila masharti na mwekezaji au mtu yeyote anayeitaka afike kuinunua na atakuwa na hiari ya kuiacha timu hiyo Mtwara au kuipeleka mkoa wowote.

BAADA YA KUPEWA ‘UKOCHA MKUU’ KWA MUDA….HIZO TAMBO ZA MATOLA KWA MBEYA CITY UTAFIKIRI MOURINHO AISEE… DAH…IDDI NADO NDIO BASI TENA AZAM FC….DAKTARI ADAI OPERESHENI YAKE ILIKUWA KUBWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply