CAF

KUHUSU MASHINDANO YA CAF MSIMU UJAO NA TAREHE RASMI YA KUANZA..UKWELI WOTE HUU HAPA…

admin June 15, 2022 6:04 pm


Hatimaye Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limetangaza tarehe ya kuanza kwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa msimu ujao 2022/23.

‘CAF’ imetoa taarifa hizo kupitia ‘Caf Online’ ambapo imethibitika kuwa, hatua ya awali ya michuano hiyo mikubwa Barani Afrika upande wa vilabu, itaanza rasmi siku ya Ijumaa (Agosti 12).

Hatua ya makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho itanza mwezi Septemba na kumalizika Novemba 18-2022

Hatua ya Mtoano katika michuano hiyo imepangwa kuanza Mwezi Februari-2023, baada ya kumalizika kwa Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN 2023’ zitakazounguruma nchini Algeria.

Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na timu nne katika michuano ya CAF upande wa vilabu msimu ujao, ambapo Ligi ya Mabingwa kuna dalili miamba ya Simba SC na Young Africans ikashiriki, huku upande wa Kombe la Shirikisho, ikiwa bado haijafahamika hadi sasa ni timu zipi zitakata tiketi ya michuano hiyo.

BAADA YA KUONEKANA KAMA WAMESHINDWA BEI YA AZIZ KI….AHMED ALLY AIBUKA NA TAMKO HILI…ADAI NI UHUNI KWA SIMBA… KUELEKEA MSIMU UJAO….TARAJIA KUONA KIUNGO HUYU MJANJA MJANJA AKIKIPIGA MSIMBAZI…NI ZAIDI YA MIQUISSONE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply