Habar za Usajili Simba

KUELEKEA MSIMU UJAO….TARAJIA KUONA KIUNGO HUYU MJANJA MJANJA AKIKIPIGA MSIMBAZI…NI ZAIDI YA MIQUISSONE…

admin June 15, 2022 6:09 pm


Klabu ya Simba SC imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu ya Bechem united FC ya Ghana Augustine Okrah.

Taarifa zilizopatikana leo Jumatano (juni 15) zinaeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ana nafasi kubwa ya kutua Msimbazi mwishoni mwa msimu.

Okrah atasaini mkataba na Uongozi wa Simba SC wa miaka miwili, huku kukiwa na kipengele kidogo cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, kama mambo yatamnyookea katika msimu wake wa kwanza.

Okrah ambaye ana sifa ya kucheza kwa kasi huku akiwa na ujanja ujunja mwingi wa kuihadaa safu ya ulinzi ya timu pinzani, amefunga mabao 14 katika michezo 31 kwenye Ligi Kuu ya Ghana msimu huu 2021/22.

Hadi msimu wa soka nchini Ghana unamalizika Okrah alikua miongoni mwa wachezaji waliotajwa sana, kuwa na kiwango bora na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakawana Tuzo katika Ligi ya nchi hiyo kwa msimu huu 2021/22.

KUHUSU MASHINDANO YA CAF MSIMU UJAO NA TAREHE RASMI YA KUANZA..UKWELI WOTE HUU HAPA… PAMOJA NA KUPATA KAZI UARABUNI…ADEL ZRANE AENDELE KUANIKA MAPYA KUHUSU SIMBA…ADAI ANAJUA YOTE …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply