Habari za michezo

KUHUSU ULE MPANGO WA KUSAJILIWA NA YANGA….KAMBOLE KAANIKA YOTE WAZI…”LAKINI NAKUJA….”

admin June 15, 2022 2:18 am


MSHAMBULIAJI raia wa Zambia, Lazarous Kambole, amefichua kuwa, suala lake la kujiunga na Yanga lipo chini ya wakala wake, lakini muda si mrefu atakuwa mchezaji wa timu hiyo.

Mzambia huyo anatajwa kumalizana na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kaizer Chief ya Afrika Kusini ambapo amemaliza mkataba wake.

Ikumbukwe hii siyo mara ya kwanza kwa Yanga kumtaka mshambuliaji huyo ambapo msimu uliopita walishindwa kufikia muafaka kutokana na dau lake la usajili kuwa kubwa hali iliyofanya Yanga kukaa pembeni kabla ya kumrejea tena mwaka huu.

Akizungumza moja kwa moja kutoka kwao Zambia, Kambole alisema kila kitu kipo sawa, hivyo ni jambo la muda yeye kutua Yanga.

“Hapa tunavyozungumza nimekuja hospitali kumleta mtu, lakini kitu ambacho naweza kukwambia kwa sasa mambo yote yanakwenda sawa maana wakala ndiyo yupo katika kushughulikia vitu vya mwisho, hivyo ni jambo la kusubiria.

“Siwezi kusema ni kwa muda gani wamekubaliana huo mkataba, niache kwa sasa halafu nitarejea kwako kukueleza kila kitu, lakini nakuja Yanga,” alisema Kambole huku akionekana mwenye furaha.

UJENZI WA UWANJA SIMBA MAMBO YAANZA KUWA MATAMU…BARBARA ATAKA VIWANJA VINNE KWA MPIGO….MPANGO UKO HIVI… SAKATA LA MIQUISSONE KURUDI MSIMBAZI…BOSI MZITO SIMBA AIBUKA NA HILI JIPYA….AFICHUA A-Z UKWELI WA MAMBO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply