Habari za michezo

BAADA YA KUVULIWA UBINGWA JANA…SIMBA ‘WAKUBALI KUCHUTAMA’….WAIPIGIA SALUTI YANGA ..WAJIBIWA HIVI…

admin June 16, 2022 2:33 pm


Muda mfupi baada ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kuweza kufanikisha lengo la kuwa mabingwa watani zao wa jadi Simba wametuma ujumbe wao.

Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa umewafanya Yanga kusepa na pointi tatu na kufikisha pointi 67 ambazo hizo ni mali yao na hazitafikiwa na timu yoyote.

Ikumbukwe kwamba Yanga bado haijapoteza mchezo ndani ya ligi licha ya kumenyana na Simba mara mbili kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza na ile ya pili zote waligawana pointi mojamoja bila kufungana.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram Simba wameandika namna hii:”Tunawapongeza Yanga SC kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2021/22,#NguvuMoja na kuusindikza na picha ya Yanick Bangala beki wa Yanga na Chris Mugalu wa Simba.

Yanga hawakuwa na ajizi nao waliweza kudondosha ujumbe wao kwa kusema:”Asante Mtani’.

Yanga inatwaa ubingwa wa 28 wa ligi ikiwa ni baada ya kuyeyuka misimu minne mfululizo kwa kushuhudia kombe linakwenda kwa watani zao wa jadi Simba.

JEMEDARI : ULEMAVU WA MANARA USIWE KINGA YA YEYE KUDHIHAKI WENGINE…ALIMDHIHAKI BOSI WAKE ANA KILO 800… PAMOJA NA KUDORORA MSIMU HUU…SIMBA WAZIDI KUTAKATA VIWANGO VYA CAF….YANGA HAIONEKANI ETI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply