Habari za michezo

RASMI….MANARA AMATAMBULISHA MORRISON YANGA…ATUMIA NJIA YA ‘KININJA’ KWA KUMTAJA KUWA MCHEZAJI BORA….

admin June 16, 2022 1:46 am


MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema kuwa kulingana na mafanikio waliyokuwa nayo klabu ya Yanga msimu huu kikosi bora cha msimu kwa mtazamo wake kinatakiwa kiwe na wachezaji zaidi ya 7 hadi 9.

Msemaji huyo ameongezea kwa kusema kuwa mchezaji wa Simba Bernard Morrison naye anastahili kuwemo kwenye kikosi hicho licha ya kucheza michezo michache ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Alipoulizwa kwanini Bernard Morrison, wakati amecheza michezo michache? Manara alijibu kuwa Bernard Morrison ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee na ubora mkubwa unaomfanya aingie kwenye kikosi hicho.

Hata hivyo, habari za uhakika ni kuwa tayari Yanga wameshamalizana na Morrison, ambapo kilichobaki ni kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania.

Morrison anatarajiwa kutangazwa Yanga Mwishoni mwa msimu huu, ili kuiepusha klabu hiyo na malipo ya kuvunja mkataba baina yake na Simba.

Kwa mantiki hiyo, Manara anawaandaa kisaikolojia mashabiki wa Yanga kuwa wajiandae kwani nyota huyo kuanzia msimu ujao ni mali yao.

A-Z JINSI YANGA WALIVYOICHAKATA COASTA UNION JANA….MAYELE ATETEMA KWA HASIRA…CHICO KAONA MWEZI…. KISA BARBARA KUIANZA ‘PROJEKTI’ YA UWANJA SIMBA….RAGE AIBUKA NA HILI JIPYA…ADAI TIMU INATUMIA GHARAMA KUBWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply