Home Habari za michezo KISA USAJILI WA AZIZ KI….MANARA AFUNGUKA HAYA…ADAI YUKO TAYARI KUACHA KAZI YANGA…”MTAJUA...

KISA USAJILI WA AZIZ KI….MANARA AFUNGUKA HAYA…ADAI YUKO TAYARI KUACHA KAZI YANGA…”MTAJUA UKWELI WOTE”….


SAKATA la usajili wa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Stephanie Aziz Ki, limeingia katika sura mpya na kumuibua Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye amefunguka kila kitu kuhusu ishu ya staa huyo kutua Jangwani.

Aziz Ki amekuwa gumzo kubwa kwa siku za karibuni kufuatia kuziingiza kwenye vita kali klabu za Simba na Yanga ambazo zote zimeonesha nia ya kuhitaji saini yake, ambapo inaelezwa kuwa tayari Yanga wamemalizana naye.

Staa huyo alijiunga na ASEC Mimosas Januari 2021, ambapo kwenye michuano ya kimataifa pekee msimu huu wa 2021/22 ameifungia timu hiyo mabao manne akicheza michezo 10.

Akizungumzia usajili wa staa huyo ndani ya Yanga, Manara alisema: “Unajua watu wengi wanakosea, sisi hatujaanza kumfuatilia Aziz Ki mara baada ya kucheza dhidi ya Simba, tumeanza kumfuatilia tangu Agosti mwaka jana ila kilichokwamisha ni kwamba tayari alikuwa amesaini mkataba na ASEC.

Aziz Ki anahushishwa na dili la kujiunga na Klabu ya Yanga

“Wakati Simba wanavutiwa na mchezaji huyo, tayari Injinia Hersi alikuwa ameshaanza mazungumzo naye, lakini kuna watu wanahoji kwa sababu wanataka picha na wengine wanadai wamemsajili.

“Sasa niwaweke wazi kuwa wekeni kumbukumbu hii, ifikapo tarehe 28, saa sita usiku kuelekea tarehe 29 saa sita na dakika moja tutajua nani mkweli, mimi niko tayari kuacha kazi Yanga.”

Wikiendi iliyopita, zilisambaa picha zikimuonesha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said, akiwa na Aziz Ki sambamba na wakala wake walipokutana nchini Ivory Coast.

Picha hizo zilionesha wazi kuna mazungumzo baina yao juu ya masuala ya kuingia mikataba na kuzua gumzo kubwa.

SOMA NA HII  SIMBA YATAMBA TENA AFRIKA...SAKHO AFUATA NYAYO ZA MIQUISSONE KWA UBORA CAF...