Habari za michezo

BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI WAKE NA SIMBA…MOSES PHIRI AZIDI KUYAWEKA WAZI MAHABA NIUE YAKE KWA MNYAMA…

admin June 18, 2022 2:52 pm


Nyota mpya wa klabu ya Simba Moses Phiri, amefunguka kuwa ndoto yake imetimia baada ya kufanikiwa kutua katika kikosi na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Phiri raia wa Zambia amesema Simba ni timu kubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati na alitamani siku moja kucheza hapa ingawa amefuatwa pia na timu nyingine za hapa nchini.

“Ndoto yangu imetimia, nilikuwa natamani kucheza soka la Tanzania. Timu kadhaa zilinifuata lakini nimeichagua Simba. Marafiki zangu (Clatous Chama na Rally Bwalya) waliniambia kuwa hii timu kubwa na menejimenti yake ni nzuri na iko makini,” amesema Phiri.

Phiri ameongeza kuwa anajua Simba ni timu kubwa inashiriki michuano mikubwa inagombania ubingwa wa ligi kila msimu na mashabiki wanahitaji furaha lakini hana presha kwa kuwa soka ni kazi yake.

Kuhusu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ambao malengo yetu ni kufika nusu fainali, Phiri amesema kwa kushirikiana na wachezaji wenzake na benchi la ufundi anaamini tutafikia matarajio yetu.

STAA ANAYETAJWA KUTUA SIMBA ASHINDA TUZO SITA LIGI YA UGANDA…NI KIFAA HATARI NA NUSU AISEE.. POGBA AIAGA MAN UNITED KWA ‘KICHAMBO CHA KIZARAMO’…ADAI ATAWAKOMESHA WAONE KUWA WALIMKOSEA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply