Habari za michezo

KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA…KASHAFUNDISHA KLABU 13 ZA AFRIKA…REKODI YAKE NI KILIO NA MAJONZI TUPU…

admin June 20, 2022 2:06 pm


Uongozi wa Klabu ya Simba SC upo katika hatua za mwisho kumuajiri Kocha kutoka nchini Slovakia Josef Vukuzic mwenye UEFA PRO License A.

Inaelezwa kuwa mazungumzo ya pande hizo mbili yamefikia pazuri, na huenda mambo yakakamilika ndani ya juma hili, na Kocha huyo kutangazwa kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC.

Josef alianza kazi ya ukufunzi wa soka mwaka 1999, amezunguka katika vilabu mbalimbali takribani 13 na Barani Africa amefundisha vilabu 4 (Al ahly Benghazi, Cape Town City, Polokwane na Amazulu).

Mwaka 2018 alifundisha Polokwane City na kuwaongoza kumaliza katika nafasi ya tano akatimuliwa na kujiunga na Amazulu FC 2019, ambayo aliwaongoza katika Michezo 20 tu, na akaondoka huku sababu zikitajwa kutoelewana na wachezaji pamoja na matatizo ya COVID 19.

Kwa sasa Kocha Josef anakinoa kikosi cha klabu ya Kosice ya Slovakia, ambapo amekiongoza katika Michezo 33 akishinda mechi 19 akipata Sare 5 akipoteza 9.

Josef, anatumia mfumo wa 4-3-3 hajawahi kuipa klabu ya Africa Ubingwa wa Ligi na hata kufikisha hatua ya juu katika mashindano ya kimataifa.

KILICHOIGHARIMU SIMBA MSIMUU CHATAJWA….MALOTA AFUNGUKA KILA KITU…ADAI ILIKUWA LAZIMA IWE HIVYO… KISA UBINGWA WA YANGA…MASAU BWIRE KAANIKA MBIVU NA MBICHI HALI ILIVYOKUWA…”GSM HANA MKONO WA BIRIKA”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply