Habari za michezo

MANARA: KUNA WATU WANATAKA KIKI KWA JINA LANGU…NILIPOFIKIA KIMAFANIKO WAO HATA NDOTONI HAWAJAFIKA…

admin June 21, 2022 2:39 am


Kutoka kwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Mabingwa wa Kombe la NBC Premier League, Haji Sunday Manara kuhusu bifu lake la baadhi ya waandishi wa habari ambao amekuwa akidai kuwa wanamsema vibaya na kuisema Yanga.

“Ruhusu wakuseme ili wajulikane, bila wewe hakuna kiki mjini, ruhusu wajaribu kukushusha ili na wao wapande, ruhusu jina lako liwe ajenda yao ya kila siku ili na wao wasikike.

“Bila kukudiss wewe mitandaoni, likes na comments ni za kutafuta, bila kukudiss wewe redioni hawasikiki.

“Muhimu usikubali kutoa kiki nyingine, ulizotoa zimetosha, usiwe rahisi kuwapa umaarufu Kwa kutumia jina lako. Itoshe sasa kuhangaika na kazi yako, unao ufuasi mkubwa mitandaoni, waache fans watashughulika nao.

“By the way lini ushawahi kuangushwa na ngonjera za mitandaoni? Sana sana endorsements zinazidi kuongezeka na mafanikio kikazi hakuna anaekusogelea.

“Ulipofika wewe wao hata ndotoni hawajahi kufika, ukiwajibu tena nitakuona mtu wa hovyo kuliko wao, unadhani na wao hawahitaji kufika ulipo? ‘Why ujibizane nao mwanangu? ‘Alimaliza kuniusia jirani yangu ambae ni Mzee wa makamo asubuhi hii. Nimepokea,” amesema @hajismanara.

PAMOJA NA KUICHARANGA KMC KWA HASIRA JUZI…MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA KWA ALICHOKIONA…ADAI WALISUMBUA… HIVI NDIVYO MAYELE ALIMVYOZIDI KUIGARAGAZA SIMBA…AVUNJA REKODI HII NYINGINE KUBWA YA STAA WAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply