Habari za michezo

PAMOJA NA KUICHARANGA KMC KWA HASIRA JUZI…MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA KWA ALICHOKIONA…ADAI WALISUMBUA…

admin June 21, 2022 2:33 am


Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola, amesema ushindi walioupata jana dhidi ya KMC walistahili kutokana na kiwango kikubwa kilichooneshwa na wachezaji wake. Matola amesema timu yake ilicheza vizuri muda wote na wachezaji walijitahidi kufuata maelekezo aliyowapa.

Matola ameongeza kuwa, kipindi cha kwanza KMC waliingia kwa njia ya kuzuia hivyo wote wakawa nyuma ya mpira lakini kipindi cha pili walivyofunguka waliweza kuwafunga.

“Ukiangalia mchezo mzima sisi tulikuwa bora zaidi yao, tulitengeneza nafasi nyingi na tulistahili kupata ushindi kwa kuwa tulicheza vizuri.

“KMC walitusumbua kipindi cha kwanza kwa kuwa wote walikuwa nyuma ya mpira walikuwa wanazuia tu lakini tulivyorudi cha pili tulitafuta njia za kuwafungua na kufanikiwa kupata mabao yote matatu,” alisema Matola.

RASMI…BAADA YA KUPAMBANA VYA KUTOSHA UBELIGIJI….SAMATTA ARUDI TIMU KUBWA ULAYA….SAFARI NZIMA IKO HIVI… MANARA: KUNA WATU WANATAKA KIKI KWA JINA LANGU…NILIPOFIKIA KIMAFANIKO WAO HATA NDOTONI HAWAJAFIKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply